HABARI: Rais Magufuli leo September 11 ameteua Mwenyeviti wawili

Leo September 11, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. John Stanslaus Ndunguru kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA). Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Ndunguru umeanza tarehe 09 Septemba, 2019. Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Prof. Antony Manoni Mshandete kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA). Prof. Mshandete ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Utafiti na Ubunifu), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kilichopo Mkoani Arusha.

Share:

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Total Pageviews

Search This Blog

Powered by Blogger.

Search This Blog

AUDIO

About Me

My photo
Nyamagana City, Mwanza, Tanzania

Labels

Blog Archive

Recent Posts