DUA zinahitajika kutokana na madai kwamba, nyota wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando amelazwa hospitalini nchini Kenya, katika chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’, Risasi Mchanganyiko limedokezwa.
Chanzo makini kutoka nchi hiyo jirani kilieleza kuwa, hali ya mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kibao kama Nibebe, Nipe Uvumilivu na nyingine nyingi kwa sasa yupo hospitali akisumbuliwa na maradhi ikiwemo mikono inayotajwa kuwa imeharibika. Kilieleza kuwa, baada ya Rose kushindikana kupata nafuu kanisani alikokuwa anafanyiwa maombi, mwenyeji wake ambaye naye ni mwimbaji wa injili pamoja na wenzake walimpeleka hospitali (haikutajwa) kwa tiba zaidi.

Kwa sasa yupo ICU huku Kenya ambapo suala la afya yake liko mikononi mwa baadhi ya waimbaji Injili wa huku ambao wamekuwa wakifanya siri ili watu wasijue kama Rose kalazwa.
“Ukweli haujulikani kalazwa hospitali gani, lakini kuna madai kuwa ameathiriwa sana na madawa ya kulevya hivyo wanahofia wakitaja jina la hospitali kila mtu atajua chanzo cha kuumwa kwake.
No comments:
Post a Comment